Language services - Kiswahili (Swahili)
Translated resources
Fasil ya kivinjari (chagua kichupo) (Browser translation (Choose tab))
-
Kanusho (Disclaimer)
-
Safari (Safari)
-
Google Chrome (Google Chrome)
-
Microsoft Edge (Microsoft Edge)
Idara ya Hazina ya Michigan haiwajibiki kisheria kwa uharibifu au madhara yoyote yanayoweza kusababishwa na matumizi ya tafsiri zozote zinazotolewa na programu au kivinjari cha wahusika wengine. Matumizi ya huduma yoyote ya muhusika mwingine itakuwa ni hiari ya mtumiaji pekee. Taarifa zinazohusiana na huduma za wahusika wengine hutolewa kama zinafaa pekee.
Safari hutoa tafsiri katika Kiarabu, Kichina (Kilichorahisishwa), Kifaransa, Kijerumani, Kiitaliano, Kijapani, Kikorea, Kireno, Kirusi, na Kihispania.
Eneo-kazi (desktop)
1. Fungua kivinjari cha Safari na uchague Vie, kisha Tafsiri kwenye menyu kunjuzi.
2. Weka kivinjari chako katika lugha inayopendelewa, ambayo si Kiingereza.
3. Nenda kwenye ukurasa wa tovuti unaotaka kutafsiri.
4. Kitufe cha kutafsiri kitaonekana upande wa kulia wa upau wa anwani. Huenda tafsiri zisipatikane kwa kurasa zote.
5. Chagua kitufe cha kutafsiri na lugha unayoipendelea.
iPhone au iPad (iPhone or iPad)
1. Fungua kivinjari cha Safari kwenye kifaa chako cha mkononi na uende kwenye ukurasa wa tovuti unaotaka kutafsiri.
2. Chagua alama ya "aA" iliyo karibu na upau wa anwani ili kuona machaguo ya tovuti. Kwenye menyu kunjuzi, chagua Tafsiri kuwa na lugha unayopendelea.
3. Chagua Washa Tafsiri ikiwa menyu ibukizi itaonekana. Kumbuka kwamba utaombwa kuwasha tafsiri mara moja pekee.
Vifaa vya Apple vyenye mifumo endeshi ya zamani zaidi ya IOS 14.0, haitajumuisha kipengele hiki. Pakua programu ya Google Translate au programu ya Microsoft Translator kwenye kifaa chako ili kupata tafsiri.
Eneo-kazi (desktop)
1. Fungua kivinjari cha Chrome na uende kwenye ukurasa wa tovuti unaotaka kutafsiri. Menyu ibukizi ya Tafsiri ya Google inaweza kuonekana chini ya upau wa anwani.
2. Chagua lugha unayoipendelea kwenye menyu ili kutafsiri ukurasa huo.
3. Ikiwa menyu ya kutafsiri haionekani, chagua kitufe cha Google Translate kilicho upande wa kulia wa upau wa anwani. Chagua lugha unayoipendelea kwenye menyu ili kutafsiri ukurasa huo.
4. Ili kupata lugha nyingi zaidi kwa ajili ya tafsiri, chagua kitufe cha Google Translate kilicho upande wa kulia wa upau wa anwani, kisha chagua alama ya menyu ya kitendo.
5. Kwenye menyu kunjuzi, teua Chagua Lugha Nyingine na uchague lugha unayopendelea kwenye menyu kunjuzi.
Simu au kishikwambi cha Android (Android phone or tablet)
1. Fungua kivinjari cha Chrome kwenye kifaa chako cha mkononi na uende kwenye ukurasa wa tovuti unaotaka kutafsiri.
2. Menyu ya Tafsiri ya Google inaweza kuonekana chini ya skrini.
3. Chagua lugha unayoipendelea kwenye menyu ili kutafsiri ukurasa huo.
4. Ili kupata lugha nyingi zaidi za kutafsiri, chagua alama ya menyu ya vitendo na uchague Lugha Zaidi kisha chagua lugha unayoipendelea kwenye menyu kunjuzi.
- Unapofungua kivinjari cha Microsoft Edge, chagua nukta tatu kwenye kona ya juu kulia ya kivinjari chako kisha, chagua Mipangilio kwenye orodha kunjuzi.
- Chagua Lugha, upande wa kushoto wa dirisha la kivinjari chako na uweke lugha unayoipendelea kwa kuchagua Ongeza lugha na kufuata vidokezo.
- Ukitembelea ukurasa ambao haujatafsiriwa katika lugha unayoipendelea, menyu ibukizi ya tafsiri inaweza kuonekana kwenye upau wa anwani.
- Fuata vidokezo ili kuchagua lugha unayoipendelea na uchague Tafsiri ili kutafsiri ukurasa huo.